Journal Swahili Matin, 15 Juillet 2026.

Waganga kunako kituo cha afya ya huko Rwampara mji Bunia wakazia mgomo wao wa kazi. Ikiwa ni wao watumika kunako kituo cha kutibuwa Ebola, wadai malipo ya mshahara wao.

Kipi kugeuza utajiri ya ardhi kuwa fursa ya kupata amani ? hii ni swali anayo simamiya waziri wa mambo ya inje inchini,  Thérèse Kayikwamba Wagner, kunako baraza kuu ya usalama ya umoja wa kimataifa.

Wakati huo hali ya hoihoi yaripotiwa huko Kalemie kulingana na uwepo wa umati wa jeshi la taifa kunako vitongoji vingi mjini. Tayari msako ya kuwashika umeanjishwa.

/sites/default/files/2026-07/150726-journal-swahili-matin-00.mp3