Journal Swahili Matin, 24 Juillet 2026

Mbele ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inaendelea kutetea mpango wa kuleta amani mashariki mwa nchi. Hii kupitia kumaliza uporaji haramu wa mali ya Congo na kukomesha mitandao inayochochea makundi yenye silaha.

Mjini Matadi, wafanyabiashara katika soko la Ango-Ango/Noki Wanapinga uamuzi wa mamlaka wa kuhamisha eneo lao la biashara. Soko hiyo inawapokea wafanya biashara wadogowadogo kati ya DRC na Angola.  

Na jimboni Kasai Central, Shirika la Kitaifa la Huduma za Umeme Vijijini na Maeneo ya Pembezoni mwa Miji (ANSER) limeviwekea vituo saba vya afya kisima cha maji, mfumo wa umeme wa jua, na vifaa vya computer. Lengo ikiwa ni kuboresha huduma kwa wagonjwa katika eneo hilo.  

/sites/default/files/2026-07/24072026_-_jp_sw_-_matin_-_00.mp3