Journal Swahili Soir, 09 septembre 2026.

Bado mji mkuu Kinshasa, msongamano wa magari unaongezeka kutokana na baadhi ya madereva kutoheshimia kanuni ama sheria za barabara. Madereva hao wanaoingia kwenye njia ya magari yanayo kuja ngambo, wanazuia kabisa usafiri katika baadhi ya barabara.

Huko Kongolo, jimboni Tanganyika kiongozi wa watu wanaodaiwa kuwa wanamgambo amekamatwa pamoja na watu wengine. Viongozi wanasema watuhumiwa hao watasambishwa na vyombo vya sheria.

Katika mkoa wa Tshopo, walimu wa Basoko na Yahuma hawajalipwa mishahara tangu mwezi  wa sita. Muungano wao unaomba viongozi kuingilia kati ili kutatua hali hiyo.

/sites/default/files/2026-09/090926-p-s-_journal_sw_soir-00.mp3