Jimboni Ituri, wapiganaji wa Codeco walishambulia magari mengi ya usafiri karibu na kijiji cha Dhera, kwenye Barabara Kuu nambari 27 katika mtaa wa Djugu. Huko waliwapokonya abiria mali zao na kiasi kikubwa cha fedha.
Na kuhusu janga la Ebola, Baraza la Kitaifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na yanayo fanya kazi ya Kibinadamu nchini DRC (CONAFOD-RDC) linasema kwamba ili kushinda Ebola, inabidi kutegemea zaidi mashirika za mahali ili kuwaleta wakaaji kuaminia mipango yote ya kupambana na janga hili.
Wakati huu mjini Mbuji Mayi, hofu imerejea katika kata la Masengu Kanyinda ambako vijana wahalifu wanaojulikana kama "Zabalo" wameanza tena vitendo vyao. Kila jioni, vijana wale washambulia wanawake wanaotoka sokoni, na kuwapokonya mikoba, simu, na vingine vifaa vya samani.
/sites/default/files/2026-07/20072026_-_journal_swahili_-_soir_-_00.mp3







