Journal Swahili Vendredi Matin, 14 aout 2026

Kivu kusini, jeshi la taifa la Kongo pamoja na Wazalendo waziteka upya vijiji vya Lumbishi na kandokando mtaani Kalehe. Ni kihisha mapambano makali zidi ya mashambulizi ya waasi wa AFC/M23, huripoti msemaji wa kanda la 34 la jeshi.

Inchini DRC, mlipuko huu mpya wa Ebola waweza fikia kuwa mkubwa zaidi kuliko hizo zilizopita. Shirika la afya ulimwenguni, WHO, latoa maoni haya wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari Jumatano mjini Geneva...

Wanabunge wa jimboni na wale wa taifa wachaguliwa wa Lwiza waombwa kuwasili huko wakati huu wa likizo. Mwito watolewa na shirika jipya la Kiraia tawi la eneo lile la Jimbo la Kasai central.

/sites/default/files/2026-08/140826-sw-journal-complet-vendredi-matin-00.mp3