Journal matin

Habari za siku ya pili asubuhi

 

  • Waziri wa Kongo aneyehusika na  Haki za Binadamu anasema kwamba inchi ya Kongo imejitolea kabisa kwa  kukuza haki za binadamu kwa mtazamo kamili.
  • Katika jimbo la Kwilu, ma adui  wawili wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya wakuu wa  vijiji vya BUKUSU na FADIAKA, waliokamatwa katika eneo la Bagata walipelekwa  siku ya kwanza mjini   Bandundu.
  • Katika jimbo la Kivu ya Kasakazin, Msemaji wa operesheni za kijeshi  Sokola ya kwanza   anatoa wito kwa wakaadji  wa Butembo na eneo zima kuwa waangalifu  ili kupambana  na tishio la kigaidi .
  • Katika jimbo la Kivu ya Kusini … kuliandaliwa siku ya pili hii  siku bila kazi yoyote katika mtaa na mji wa Uvira na vile vile katika mji wa  Sange.
  • Huko Ituri, vituo saba vya redio za jamii katika mtaa wa  Mambasa, karibu kilomita mia moja makumi sita  na tano kutoka mji wa Bunia, vimepewa vifaa vya mawasiliano na shirika lisilo la kiserikali la Search For Common Ground.
  • Inchi ya Kongo ya Kidemokratisa inakuwa kwa sasa  sawasawa  na Indonesia na Brazili katika mkakati wa kugombea  haki za wakazi wake.
  • Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, Prince Kihangi,  mwanabunge jimboni  anapendekeza mtaa wa walikale ushurutishwe na mradi wakupewa mkopo wa kaboni .
  • Jimbo Kivu Kusini, kilalo cha  muda cha  Cihanda katika eneo la  Nyangezi mtaani Kabare kilizinduliwa  siku ya pili/sites/default/files/2022-10/051022-p-s-kinjournalswahilimatingraceamzati-00_web_0.mp3