Journal matin

Habari za siku ya pili asubuhi 

  • Kikao cha mwisho cha awamu ya tatu ya mchakato wa amani mashariki mwa DRC kilichopangwa kumalizika hii siku ya kwanza, kitafanyika hii siku ya pili huko Nairobi inchini Kenya. Uamuzi ni wa rais wa zamani wa Kenya na mwezeshaji wa mchakato huu.
  • Waziri Mkuu Sama Lukonde alikabithi Waziri wa Masuala ya Kijamii, Mshikamano na Hatua za Kibinadamu, Modeste Mutinga siku ya kwanza hii tarehe tano Desemba, hapa Kinshasa, kartasi ya kuchukua pesa kwenye bengi yenye Franga za Kongo bilioni mia mbili.
  • Huko Kivu Kaskazini, utulivu ulionekana  wikendi yote, hadi siku ya kwanza hii kwenye uwanja wa mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la Kongo.
  •  Askofu wa dayosisi ya Katoliki ya Butembo-Beni anasema ana wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya usalama katika mji wa Butembo.
  • Jimboni Ituri, askofu wa  dayosisi ya katoliki ya Bunia analaani uporaji wa rasilimali za jimbo hilo unaofanywa na wageni na baadhi ya Wakongo.
  • Kampeni ya Siku kumi na sita za Kupinga Ukatili wa Kijinsia inaendelea bila kusitishwa kote nchini. Pa Kinshasa, Bi Tyna Likula, mwanachama wa Mtandao wa viongozi wanawake kwa ajili ya kupewa neno, moja wa viongozi katika Wizara ya Mawasiliano na vyombo vya habari, alifikiri Jumapili, tarehe ine Desemba, kwamba wenzake lazima wafanye kazi kwa bidii ili kustahili nafasi za uwajibikaji katika kazi zao.
  • Miezi miwili hivi, mafuriko yanaendelea kuvuma katika maeneo mengi ya Equateur. Ni kutokana na mvua kubwa inayonyesha kila siku katika eneo hilo. Mvua nyingi kiasi kutokana na hali yake katika pande zote za mstari wa Equateur.
  • Huko Kasaï-Oriental, bei ya mahindi imeongezeka katika masoko ya jiji la Mbuji-Mayi. Kipimo cha kilo tatu na nusu za mahindi kwa sasa kinauzwa franga za Kongo elfu saba na mia tano lakini wiki mbili zilizopita kipimo hicho kilikuwa kikiuzwa kwa franga elfu tano za Kongo./sites/default/files/2022-12/06122022-p-s-journalswahilimatin-00_web.mp3

Recevez Radio Okapi par email

Donnez votre adresse email dans ce formulaire afin de recevoir tous nos articles dans votre boîte email. Vous recevrez un message de confirmation avec un lien sur lequel il vous faudra cliquer afin que l'envoi d'emails devienne effectif.
Si vous ne voyez pas l'email de confirmation dans votre boîte de réception, allez chercher dans vos spams et marquez le message comme "non spam".  

Votre adresse email :

Service offert par FeedBurner