Journal Soir

Habari za siku ya tatu jioni

 

  • Katika jimbo la Kwilu, msimamizi wa mtaa wa Bulungu ametoa  tangu siku ya kwanza amri ya kutokutembea usiku  katika eneo helo.
  • Miaka minane ya mauaji katika mtaa  wa Beni ni mingi , oparesheni za kweli za kuwasaka waasi ni lazima zifanyike .
  • Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini: Mwezi mmoja baada ya kuanza kwa mwaka wa shule,  watoto wengi bado hawajarejea shuleni katika mtaa wa Rutshuru.
  • Jimboni, Kivu ya Kusini, watoto makumi mbili  na sita walikuwa kwenyi makundi yenye kumiliki  silaha wametenganishwa na makundi hao  katika mtaa wa Mwenga .
  • Huko Kamanyola, katika mtaa wa Walungu jimboni Kivu ya  Kusini,  shughuli zilianza tena  tangu jana  siku ya pili jioni baada ya siku mbili  ya mzozo na maandamano ya waakadji  baada ya mauaji ya  kijana mfanyabiashara.
  • Muungano wa vikundi vya kanisa mbalimbali wenye kushurlikia ulinzi wa pori mbalilmbali inchini Kongo IRI kwa kifupi, unependekeza kwa serikali zenye kuwakilishwa kwenye mkutano wa matayarisho ya kongamano kuhusu mamzingira Precop 27 wachukuwe amri zenye mafaa kwakungojea mwaka wa elfu mbili na makumi na tatu
  • Kwa kutarajia marekebisho ya  mpango   wa uchaguzi  wa mwaka ujao inchini Kongo , offisi yenyi kuhusika na uchaguzi Ceni imetuma timu kutafuta maeneo kwa ajili ya kuhesabu na  kuandikisha  raia watakaochaguwa katika inchi za kigeni .
  • Ni kutokana na kazi ya mwalimu kwamba nchi inaweza kusonga mbele. Kwa hiyo naomba vioongozi  kushurlikia kazi yetu  . Haya ni masemi  ya Bi Yvonne Kalehezo, mwalimu kwa zaidi ya miaka makumi tatu  mjini  Bukavu./sites/default/files/2022-10/051022-p-s-kinjournalswahilisoir-00_web.mp3