Journal Soir

Habari za siku ya tano jioni 

 

  • Katika jimbo la kwilu, watu wanne  wamefariki  miongoni mwa watu waliokimbia mzozo kati ya wa Teke na wa Yaka  kutoka eneo la kwamouth huko maindombe .
  • Kulifunguliwa jana hapa mjini  Kinshasa Mkutano wa sita wa shirika la  Wabunge wa Afrika  wanaohusika na Ulinzi na Usalama .
  • Jimboni ituri,  kiongozi  wa operesheni za pamoja ya FARDC na jeshi la Uganda UPDF  na makamu wake walijilekeza katika eneo la Boga.
  • Katika mtaa wa  Beni, shirika  ya kiraia ya eneo la  Banande-Kainama inapendekeza doria  ziongezwe katika vijiji vya Banande Kainama
  • Katika jimbo la Kivu ya  Kaskazini, baraza la vijana la mtaa wa Eringeti lilianzisha  tangu siku ya kwanza   iliyopita, kazi ya kusisimua  vijana kwa lengo la  kujitahidi kwa kutafuta amani katika eneo hili.
  • Waziri anayehusika na elimu, Tony Mwaba anatangaza  kwa wakongomani wote kwa jumla  na haswa kwa wanafuzni waliofaulu kwenye  mtihani ya serikali  ya mwaka wa elfu mbili na kumi na tano  kwamba  vieti via mwisho wa shule za sekondari  vinapatikana kwenye chumba kikuu kienye kuhusika  na shule za msingi na sekondari.
  • Jimboni Kivu ya  Kaskazini, muungano ya wakaadji wa Kongo wanaofanya kazi bila malipo ASVOCO, unamuomba rais wa Jamhuri ya Kidemokratia ya Kongo  kuanzisha kazi yakuboresha sheria  .
  • Kampuni nne za uchimbaji madini zilikwenda  jana  kwenye  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, ofisi ya Lubumbashi kuzungumzia hali ya maisha ya watoto.
  • Mjini Goma, siku ya pili iliyopita,  hospitali kuu  ya jimbo la Kivu ya Kaskazini iliweza kufanya upasuaji yakuachanisha   mapacha wawili waliokuwa wakikamata kwa miezi miwili tangu kuzalika./sites/default/files/2022-10/071022-p-s-kinjournalswahilisoir-00_web.mp3