Journal Soir

Habari za siku ya tatu jioni 

  • Jimboni Kivu ya  Kaskazini, kamanda mpya wa eneo la ulinzi la tatu la FARDC na Naibu Kamanda wa Kikosi cha MONUSCO walikutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza hii siku ya tatu huko Goma.
  • Kivu Kaskazini, gavana wa kijeshi anatoa wito kwa watu waliokimbia makazi yao huko Nyiragongo watulie.
  • Kenya  ilitangaza siku ya tatu hii kutumwa kwa wanajeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kama sehemu ya uingiliaji wa kijeshi wa wilaya unaolenga kuunga mkono utawala wa Kongo katika kukabiliana na uasi unaoendelea mashariki mwa Kongo.
  • Katika  jimbo la Kivu ya Kusini maandamano makubwa ya amani yalifanyika siku ya tatu hii asubuhi katika mitaa ya BUKAVU.
  • Jimboni Ituri, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Manufaa ya Wahasiriwa wa Mahakama ya Kimataifa ya CPI yenye makao yake makuu mjini The Hague nchini Uholanzi, ambaye yuko kwenye misheni huko Bunia, anasihi kuhamasishwa kwa fedha muhimu kwa ajili ya matunzo ya maelfu ya wahasiriwa wa uhalifu uliofanywa na viongozi wa zamani wa makundi yenye silaha nchini Congo na ambao wahusika walikuwa wamehukumiwa na CPI.
  • Katika jimbo la Lomami, karibu wanafunzi mia moja wa shule ya Institut Technique Médicale de Kamiji wanasomea chini ya miti baada ya mvua kubwa kuharibu majengo ya shule wiki iliyopita.
  • Zaidi ya hekta elfu makumi sita za mahindi zimepandwa katika jimbo la Haut Katanga katika muda wa miaka mitatu kutokana na ufadhili wa kilimo uliyoanzishwa na serikali ya mkoa huo.
  • Katika jimbo la Kogo central, watu tatu waliokamatwa wiki jana huko Matadi kwa kupokea kiasi cha dola kumi kutoka kwa karibu watu elfu moja wanaofanya kazi katika sekta isiyo rasmi, sio wanamemba wa M-duka na kampuni hiyo haihakikishi chochote kwa waathiriwa wote.
  • Shirika la Fondation Bill Clinton pour la Paix linatahadharisha juu ya ongezeko la wafungwa katika magereza ya DRC, hasa gereza kuu la Makala mjini Kinshasa./sites/default/files/2022-11/02112022_-p-s-journalswahilisoir-00_web_.mp3