Journal Soir

Habari za siku ya kwanza jioni tarehe 28/11/2022

  • Rais wa Jamhuri YA Kongo alitoa wito kwa vikundi vyote vilivyo miliki silaha kuweka chini silaha zao na kujiunga na Mpango wa Kupokonya Silaha, Uhamishaji, Uokoaji Jamii na Uimarishaji, PDDRCS.
  • Kulifunguliwa siku ya kwanza  hii mjini Nairobi inchini Kenya awamu ya tatu ya mchakato wa kurejesha amani mashariki mwa DRC.
  • Katika kambi za wakimbizi kaskazini mwa Goma, kupika chakula ni tatizo. Baadhi ya watu waliokimbia makazi yao wanalazimika kuuza sehemu ya chakula chao walichopewa ili kuweza kulipia makaa au kuni.
  • "Bila ulinzi, nchi yetu itakuwepo kwa jina tu", ni nukuu ya mbunge wa kijimbo aliyechaguliwa kutoka tarafa la Beni.
  • Huko Ituri, shirika la  raia la tarafa la Mambasa liliamuru siku ya siku ya kwanza hii  kuwa siku ya mji bila kazi ikifuatiwa na kutokulipa kodi katika tarafa lote hili lililo kwa umbali wa kilomita mia moja makumi sita na tano  kusini mwa Bunia.
  • Katika jimbo la Lomami, wanabunge wa jimbo walikataa siku ya sita iliyopita, mradi wa sheria ya kijimbo kuhusu uwajibikaji wa jimbo hilo.
  • Katika jimbo la Maniema, viashiria vyote vya ukosefu wa usalama wa chakula viko juu sana.
  • Jiji la Kinshasa, linapokea kutoka tarehe makumi mbili na nane Novemba hadi tarehe mbili Desemba  vikao vya mada vya mkutano wa kwanza wa baharini wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati kupitia  mada: "Utawala na Kuwekea usalama nafasi ya bahari ya CEEAC kwa maendeleo ya Uchumi endelevu wa Bluu katika Afrika ya Kati./sites/default/files/2022-11/28112022_-p-s-journalswahilisoir_-00_web.mp3