Journal Soir

Habari za siku ya pili jioni tarehe 29/11/2022

  • Awamu ya tatu ya Mchakato wa Amani Mashariki mwa DRC: Baada ya hafla ya ufunguzi iliyofanyika hii siku ya kwanza katika Hoteli ya Safari Park jijini Nairobi, wakati sasa ni wa kuendelea na upangaji upya na usajili wa wajumbe wote waliofika hivi punde waliopo Nairobi. Kuanza kwa kazi katika vikundi na vikundi vidogo kumepangwa siku ya tatu.
  • MONUSCO inathibitisha kujitolea kwake na kuunga mkono juhudi za kidiplomasia na kisiasa ambazo zinaweza kusababisha utatuzi wa amani wa mgogoro wa mashariki mwa DRC.
  •  Katika Kivu Kusini, Daktari DENIS MUKWGE anazungumza kuhusu hali inayoendelea hivi sasa mashariki mwa DRC. Namunukuu,
  • "Ni muhimu kwamba inchi zinazosambaza silaha kwa makundi yenye silaha ambayo yamewekewa vikwazo ziadhibiwe.
  • Katika Kivu Kaskazini, mapigano makali yaliripotiwa siku ya pili hii asubuhi katika kijiji cha Kishishe.
  • Katika tarafa la Beni, hospitali kuu ya Kalunguta inafanya kazi kwa shida kutokana na kuendelea kwa ukosefu wa usalama katika eneo hilo.
  •  
  • Ukumbi wa mji wa Lubumbashi na manispaa mbalimbali zimekuwa na viongozi wapya walioteuliwa kwa amri ya rais tangu wikendi iliyopita.
  • Bunge la Mkoa wa Maï-ndombe limetangaza kukubalika kwa mradi wa sheria ya bajeti ya mwaka wa fedha wa elfu mbili makumi mbili na tatu  iliyowasilishwa na Gavana Rita Bola Dula.
  • Kulifunguliwa siku ya pili hii, makumi mbili na tisa  Novemba Jukwaa la Wasichana la DRC pa Kinshasa. Jukwaa lililoandaliwa na Unicef ​​​​chini ya mada: "Kuzungumza, kuunganisha, kuwezesha.
  • Katika jimbo la Tshopo, barabara ya taifa Namba ine, sehemu ya Kisangani-Buta, ambayo ina urefu wa kilomita mia tatu makumi mbili na ine ipo kwa jina tu./sites/default/files/2022-11/29112022-p-s-journalswahilisoir-00_web.mp3