Journal Soir

Habari za siku ya inne jioni tarehe 01/12/2022

  • Katika jimbo la Kivu Kusini, Askofu Mkuu wa Bukavu anatoa wito kwa Wakongo kuungana ili kupinga adui na kutetea udongo wote wa inchi la DRC.
  • Mwezeshaji wa EAC wa mchakato wa amani mashariki mwa DRC alipokea hii siku ya tatu makundi yote yenye silaha yanayofanya shughuli zao katika majimbo ya Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Ituri, Maniema na Tanganyika yaliyo kwenye mazungumzo jijini Nairobi.
  • Katika Kivu Kaskazini, matumizi ya nguvu imeruhusiwa dhidi ya kundi lolote lenye silaha au kundi la kigaidi linalopinga mchakato wa amani unaoendelea Luanda na Nairobi.
  • Mchakato wa Nairobi ya tatu  lazima umalizike kwa ahadi thabiti na ya dhati ya makundi yenye silaha ya Ituri katika kukomesha ukatili katika jimbo hili. 
  • Leo ni tarehe moja  Desemba elfu mbili makumi mbili na mbili, ni Siku ya kupiganisha ugonjwa wa kirusi cha ukimwi Duniani.
  • Maandamano ya wanaharakati wa chama cha UDPS, kitengo cha Tanganyika yalifanyika katika siku za hivi karibuni katika tarafa nyingi za jimbo hilo, hasa, katika eneo la Moba, Kongolo, Manono na katika jiji la Kabimba. Wanapinga uteuzi wa hivi majuzi wa viongozi  wapya wa maeneo mbali mbali.
  • Utambulisho na uandikishaji wa wapiga kura ndani ya siku makumi tisa, upangaji wa kura za moja kwa moja za Rais wa Jamhuri, manaibu wa kitaifa na wa mkoa pamoja na washauri wa manispaa ni sehemu ya mambo ya "ujasiri" na "matamanio" ya kalenda ya uchaguzi iliyotangazwa na CENI, inakadiria hivyo  Synergie des missions d’observation des élections (Symocel),  ambayo ni jukwaa la mashirika ya kiraia ya Kongo.
  • Kata nyingi za mji mkuu wa Kongo bado hazijulikani. Ni mfano wa Kata 17 Mai, katika manispaa Kisenso. Hapa, hakuna njia za lami, maji kutoka kwa regideso na hata mkondo wa umeme karibu haupo./sites/default/files/2022-12/011222-p-s-journalswahilisoir-00_web_.mp3