Journal Soir

Habari za siku ya kwanza jioni tarehe 05/12/2022

  • Katika tarafa la Rutshuru jimboni la Kivu kaskazini, miongoni mwa wahanga wa mauaji yaliyofanywa na waasi wa M23 huko Kishishe, takriban watu makumi tano wakiwemo watoto watatu waliuawa katika kanisa la mahali hapo, ambapo walikuwa wamekimbilia huko.
  •  
  • Katika eneo la Rutshuru katika jimbo la Kivu kaskazini, hali ya utulivu imeripotiwa siku ya tano hii asubuhi katika eneo la Kishishe, Kirima na Lushebere, katika tabaka Bambo, usultani wa Bwito.
  • Huko Bunia, watu wanne wa familia moja waliuawa kwa kuchomwa visu na watu wasiojulikana huko Kolomani katika Kata Mudzi-Pela.
  • Vyombo vya usalama viliwasilisha hii siku ya ine kwa gavana wa jimbo la Haut Katanga  madereva watano wa pikipiki wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya mchungaji siku ya Jumapili iliyopita katika Kata Kabulameshi huko Lubumbashi.
  • Katika jimbo la Maniema, watu kumi wanaozaniwa kuwa ni majambazi wanaotumia silaha wakiwemo wanawake wawili na askari polisi mmoja ambao wanaleta ukosefu wa usalama katika jiji la Kindu waliwasilishwa jana siku ya ine mbele ya  gavana wa muda AFANI IDRISSA MANGALA
  • Polisi ya jimbo la Kongo centrale  imepewa  na magari na pikipiki makumi tatu na ine ili kutokomeza ukosefu wa usalama katika jimbo hili.
  •  
  • Sekta ya Nishati inakabiliwa na vikwazo vingi vinavyochelewesha maendeleo yake. Miongoni mwa mizigo hii ni, kwa mfano, kodi na ushuru ambavyo havihesabiwi na serikali.  
  • Shirika la mawasiliano na uzalishaji "Les As de la presse" lenye makao yake makuu katika jimbo la Kwilu liliandaa mkutano mnamo siku ya ine tarehe moja desemba mwaka tunao kuhusu vipengele vipya katika  sheria mpya ya uchaguzi./sites/default/files/2022-12/05122022-_p-s-journalswahilisoir_-_00_web_0.mp3