Journal Soir

Habari za siku ya tatu jioni tareha 08/12/2022

  • Mkuu wa nchi Félix Antoine Tshisekedi aliwasili mjini Matadi siku ya tatu hii mwendo wa saa mbili usiku.
  • Huko Kivu Kaskazini, hali ni shwari siku ya tatu hii kwenye uwanja wa mapigano  kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23.
  • Siku ya tatu  hii katika jimbo lote la Mongala, hali ya uvamizi wa DRC na Rwanda kupitia M23 ni sababu ya maandamano ya kuungwa mkono kwa Mkuu wa Nchi, Felix-Antoine TSHISEKEDI, na kwa jeshi la FARDC.
  • Katika Kivu Kusini, wimbi la kwanza la vijana wa kujitolea waliochagua kuingiya katika jeshi waliondoka Bukavu hii siku ya pili kuelekea kituo cha mafunzo cha Kamina.
  • Huko Ituri, watu mashuhuri wa jamii za Wa Bira na Wa Hema wanatoa wito kwa wanamemba wao watulie na wasijihusishe na vurugu zinazotokana na utambulisho wao. Walisema hii siku ya pili baada ya mkutano na Gavana wa Mkoa.
  • Kulifunguliwa hii siku ya pili tarehe sita Desemba huko The Hague nchini Uholanzi majadiliano makuu wa ushirikiano wa kimahakama na matumizi ya Mkataba wa Roma na nchi wanachama kwa sheria hii inayohusiana na utekelezaji wa CPI.
  • Kulifunguliwa shughuli kuhusu za haki za mwanamke naye Innoncent Fadhili ambaye tunampokea humo studioni.
  • Vita dhidi ya rushwa duniani vinatishiwa pakubwa na visa vya utesaji bila alama na ambao waandishi wa habari za uchunguzi ni miongoni mwa waathiriwa.
  • Kusimamishwa kwa muda kwa kushuka kwa ndege kwenye uwanja wa ndege wa Bipemba huko Mbuji Mayi./sites/default/files/2022-12/07122022-p-s-journalswahilisoir-00_web.mp3