Watu makumi tatu na kenda walipotea, na wengine makumi tatu na sita wakaokolewa. Hii ndiyo matokeo ya ajali ya meli MV MJP iliyotokea asubuhi ya Jumatano kwenye Ziwa Tanganyika, karibu na mji wa Kabimba.
Amani, usalama na ulinzi wa wananchi. Hiyo ndiyo jumbe kuu yake Waziri mkuu Judith Suminwa Tuluka Jumatano mbele ya Bunge Kuu la Umoja wa Mataifa. Kiongozi wa Serikali Alitaka utekelezwe halisi wa ahadi za kikanda na za kimataifa zilizochukuliwa tayari kwa ajili ya kurejesha amani mashariki ya DRC.
Na wakulima katika manispaa ya Nsele mjini mku wa Kinshasa wanakuwa na hasira sana. Wanalaani wizi wa unao endeshwa na watu wasio julikana mashambani mwao.
/sites/default/files/2026-09/24926-bon-journal_swahili_jeudi_soir.mp3







