Journal Swahili : Soir

Wakaaji wa kijiji cha Ntemo-Ndimbanienge, yenye kupatikana mtahani Mbanza-Ngungu, wameamua kuchukua hatima yao mikononi mwao. Kwa wiki moja, wafanyakazi wa kujitolea wamekuwa wakihamasishwa kwenye barabara kadhaa za huduma za kilimo ili kuboresha hali zao.

Katika mtaa wa Demba, Kasai ya Kati, mashirika ya kiraia yanashutumu vitendo vya unyanyasaji vinavyohusishwa na baadhi ya askari wa FARDC waliotumwa katika eneo hilo. Shirika la raia  “Demba Union fait la force” unawashutumu askari wale hasa kwa kuingilia masuala fulani ya kisheria na yakimila.

Mtaani Beni, vyama vya teksi za pikipiki, vikundi vya shinikizo, na harakati za kiraia vilielimishwa kuhusu umuhimu wa mazishi ya heshima na salama kama sehemu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola.

/sites/default/files/2026-09/23926-b-s-journal_swahili_mercredi_soir_.mp3