Journal Soir

Habari za siku ya tatu jioni 

  • Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, wakaaji wa mji wa Bunagana na kijiji cha Jomba waliamka katika hali ya utulivu siku ya  tatu hii , siku moja baada ya mashambulizi ya kwanza ya anga kwenye maeneo ya kundi la waasi wa  M23 yaliyofanywa na ndege za kivita za jeshi la FARDC.
  • Chama cha Kisiasa kimachoongozwa na bwana Moise Katumbi kilitangaza siku ya pili  kuunga mkono  kwa wanajeshi wa FARDC ambao wanapiga katika mashariki mwa inchi. Kwa chama hiki cha kisiasa, inchi ya Kongo haiwezi kutiliwa shaka na lazima iheshimiwe.
  • Bunge la taifa  lilichaguwa  siku ya pili   azimio la kuizuia Serikali kuanzisha mazungumzo yoyote  na makundi yenyi kumiliki silaha ili kuwaingiza katika jeshi la serikali.
  • Jimboni la Kivu ya Kaskazini tuwajulishe kwamba raia wawili waliuawa katika shambulio jipya la waasi wa ADF usiku  wa siku ya pili wa kuamkia siku ya tatu  hii huko Kabasha, mji ulioko yapta  kilomita kumi na mnane  kutoka mji wa Beni kwenye barabara ya Beni-Butembo.
  • Ukosefu wa usalama katika mtaa wa   Bagata, hasa katika sekta ya Wamba kufuatia ukatili unaofanywa na watu wasiojulikana wenye kumiliki silaha.  Msimamizi wa eneo hili ambaye ana wasiwasi, anajiuliza jinsi gani mchakato wa uchaguzi utafanyika katika eneo hili la jimbo la Kwilu.
  • Katika jimbo la Kasaï-Central , kunaripotiwa mzozo mkali  pa Bakua Bumba, sekta ya Mwanza-ngoma, katika mtaa  wa Demba. Hali hii iliyosababisha kulunguzwwa kwa  makao machache usiku wa siku ya kwanza hadi siku ya pili , inatokana na  kutoelewana kati ya wakuu wawili wa vijiji .
  • Ziara ya Mkuu wa  Nchi Felix Antoine Tshisekedi siku ya pili  kwenye nafasi ya ujenzi wa kituo cha fedha cha mji wa Kinshasa.
  • Katika Jimbo la Tshopo, zaidi ya wafanyakazi mia nne na makumi mnane  wa offisi Kuu ya Mapato ya Tshopo wamepumuzishwa .
  • Waendesha pikipiki na madereva wa teksi na mabasi  wanakuwa tena wengi katikati ya mji wa Lubumbashi na wakisimama mahali popote hadi kufikia hatua ya kuzuia usafiri katika mji. /sites/default/files/2022-11/091122-p-f-kinjournalswahilisoir-00_web.mp3