Habari z'asubuhi 10 Juni, 2025
- Kinshasa : Mpango wa serikali ya Kongo wa kuzaa hospitalini bila malipo umeleta utata inchini. Vituo vingi vya afya vinavyotekeleza mpango huo vimeusimamisha vikidai kwamba havijalipwa tangu miezi kadhaa kwa ajili hiyo
- Bukavu : Kiwanda cha chai cha Lemera katika tarafa la Kalehe huko Kivu Kusini kimelazimika kufungwa kutokana na uporaji wa vifaa vyake vya uzalishaji na waasi wa AFC-M23. Ni kufuatana na mapigano makali kati ya waasi na Wazalendo siku ya tano iliyopita
- Goma: Huko Kivu Kaskazini, walimu wa tarafa la Masisi wanadai mishahara yao ya miezi mitano tangu mwezi Januari iliyopita. Wanailaumu Caritas, wakala wa kulipa, na wanatishia kuanzisha mgomo./sites/default/files/2025-06/100625-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3