Waziri wa Ujasiryamali na Maendeleo ya Mashirika Madogo, PME, Justin Kalumba Mwana-Ngongo, anazitaka kampuni na watu binafsi wanaodaiwa fedha za Mfuko wa Kukuza Viwanda (FPI) kulipa madeni yao haraka. Wana muda wa siku 30 kutimiza wajibu hayo.
Jijini Uvira Kivu ya kusini, watumiaji wa barabara za Uvira–Luvungi, Mwenga–Uvira, na Uvira–Fizi–Baraka wanalaani ongezeko la vitendo vya unyanyasaji, yenye kutendwa na baadhi ya wapiganaji Wazalendo. Hawa wameweka vizuizi vingi ambako wasafiri hulazimishwa kulipa pesa kaza.
Matadi, biashara ya vyuma chakavu inavutia sana vijana wenye kutafuta mapato. Tutamfata Elise KAVIRA mwenye alikutana na hawa wafanyabyashara wa vyuma.
/sites/default/files/2026-08/040826_journal-sw-mercredi_matin.mp3





