matin

Katika jimbo la Kivu Kusini, wanafunzi zaidi ya 20 wamefariki dunia katika moto ulioteketeza shule mbili. Wazazi wengi bado hawajapata taarifa kuhusu watoto wao, huku mashirika ya kiraia yakitaka watoto walio jeruhiwa watibiwe na waathirika wazikwe kwa heshima.

Jimboni Tanganyika, wafanyakazi wa kampuni ya madini Manono Lithium wame andamana kudai kuongezwa mishahara na kuboreshwa kwa maisha  yao. Shughuli za kiuchumi zilisimama kwa muda, wakati wa maandamano hayo, lakini hali imetulia tena.

Na katika jimbo ka Kivu-Kaskazini, kuongezeka kwa mapigano kati ya AFC/M23 na makundi ya Wazalendo kume zorotesha hali ya usalama na ya kibinadamu. Mashirika ya kiraia yanasema angalau vijiji 16 vimeachwa na wakazi.

/sites/default/files/2026-09/110926-p-s-_journal_sw_matin-00.mp3