
Wivine Mukata ni fundi wa kutengeneza viungo bandia, yaani ma protheses, katika kituo cha "Shirika la Umoja" kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa viungo mjini Goma.
Akiwa mwathiriwa wa vita, alipoteza mguu wake mwaka 2014 wakati bomu ilipo angukia nyumba yao pale Beni. Baada ya kutunzwa na kupewa muguu bandia na shirika la msalaba mwekundu CICR, alifaidia pia ufadhili toka shirika hilo tu kusoma kwa miaka mitatu nchini Togo; huko alijifunza kutengeneza viungo bandia ili kuwasaidia watu wengine waliopoteza viungo kutembea tena na kujenga upya maisha yao.
Katika mahojiano haya na Rosalie Zawadi, anazungumzia shida hiyo ya bomu iliyo gusa nyumba yao na kutoa wito wa kurejea kwa amani katika eneo la mashariki mwa nchi, ili watu wengine wasiendelee kuwa wahanga wa vita na kupitia mateso kama yale aliyoyapata yeye.
/sites/default/files/2026-07/25072026_-_goma_invite_sw_-_wivine_mukata.mp3








