" Ni nini turu ya pili ya uchaguzi wa uraisi ? Nani anaye husichwa na namna gani ita endeshwa ? "

Fichier audio : téléchargez Flash pour écouter.

” Ni nini turu ya pili ya uchaguzi wa uraisi, nani anaye husichwa na namna gani ita endeshwa ? ”

* Turu ya pili ya uchaguzi wa uraisi ni uchaguzi wa prezidenti wa taifa wenye uta pambanisha wagombeaji wawili walio pata sauti nyingi katika round ya kwanza.
Turu ya pili ina endeshwa wakati hakuna mgombeaji mwenye ali chinda na sauti nyingi, yaani kipande cha sauti za wachaguzi zaidi ya sauti moja.
Zamu ya pili ina kubaliwa na cheria ya uchaguzi na katiba ya taifa ya jamuhuri yakidemocrasia ya kongo.
Kuhusu wenye kushiriki katika zamu ya pili ya uchaguzi wa uraisi wa mwaka elfu mbili na sita, korti kuu ya cheria ina pashwa kuamuru, lakini matokeo ya muda yaliyo tangazwa na tume la uchaguzi huru tarehe makumi mawili ogusti iliyo pita ili taja Joseph Kabila na Jean pierre Bemba wachindi kwa turu ya pili.
Joseph Kabila ni wa kwanza na asilimia makumi mane na nne mkato makumi munane na moja na Jean Pierre Bemba wa pili na asilimia makumi mawili mkato tatu.
Kama vile turu ya kwanza ya uchaguzi wa uraisi ili endeshwa popote katika jamuhuri yakidemocrasia, ita bidi kukinga operesheni hio ya turu ya pili yenye ita chagua prezidenti wa taifa.Turu ya pili ina elekea jamuhuri yakidemocrasia ya kongo yote.Ina elekea pia walio hesabiwa na cei, wenye kuwa na kitambulisho cha watakao piga kura na wenye kualikwa kupiga kura siku ya uchaguzi.

” wakati gani zami hio ya pili ita endeshwa ? ”

* Kalendari ya Cei ina tayarisha turu ya pili ya uchaguzi wa uraisi munamo tarehe makumi mawili na tisa octoba ijao. Lakini mbele ya tarehe hio, wagombeaji wawili wana alikwa kuendesha kampeni nyipya ya uchaguzi kwa kuoenesha mara tena mbele ya wakaaji miradi yawo ya kijamii.
Juweni kwamba kufatana na habari kutoka CEI, kutangazwa kwa wagombeaji wa turu ya pili ya uchaguzi wa uraisi kutajitukiza siku moja tuu kiisha kutangazwa kwa matokeo ya mwisho ya round ya kwanza na korti kuu ya kimataifa.
rnTexte de DONAT MADIMBArnTraduit en Swahili par Jean Desire Kanyama