Habari za asubui, tarehe 09 juni 2026

Hospitali kuu ya serkali mjini Bunia yapewa msaada wa vifaa vya kujikinga kwa upekee dhidi ya maambukizi ya Ebola. Ni msaada toka jeshi la usalama la asili ya Bangadesh iliyo pokelewa na kiongozi wa hospitali hii.

Jeshi la taifa Fardc walipambana na kikundi cha wazalendo mtaani Lubutu jimboni Maniema, ikisababisha watu sita kupoteza maisha na wakaaji kuhama nyumba zao.

Huko Mbijimayi, jambo lisilo la kawaida lilianza kuonekana. Vijana wanao safisha magari waonekana kwa nafasi nyingi kunako Barabara za mji huo.

/sites/default/files/2026-06/090626-journal-swahili-matin-00.mp3