Habari za asubui, tarehe 11 juni 2026

Shirika la kutetea haki za binaadam yatowa adharani ripoti kuusu ukeukuaji wa haki za binaadam zilizo endeshwa na jeshi ya inchi ya Rwanda na waasi wa M23, ususan, kuorodheshwa pasipo kutaka, kushikwa mbali na kanuni ya kivita kwa ma elfu ya wapiganaji walio shikwa mateka na hasa wakaaji pande mwa mashariki mwa inchi DRC

Wakati huo jimboni Ituri, wahanga tisa wa janga la Ebola waondoka vituoni vya matibabu tayari wakisha tibuwa kunako hospitali ya NYAKUNDE mtaani Irumu na huko MUNGWALU mtaani Djugu. Hawa wajiongeza kunako idadi ya wengne wasio punguwa kumi hivi, walio tibiwa hivi majuzi toka janga lile.

Na wanamemba wa baraza la bunge jimboni Kasai ya mashariki wame alikwa mjini Kinshasa naye waziri ahusikae na maswala ya ndani kiserkali, ikiwa tangu ijumaa uliopita, kikao kikuu cha baraza hii iligeuzwa kuwa nafazi ya vurugo na malumbano makali, wakati ulipo hitajika uchunguzi wa kazi kunako utaratibu wa uongozi wa jimbo.

/sites/default/files/2026-06/110626-jrnl-swahili-matin.mp3