Habari za asubui, tarehe 12 juni 2026

Zaidi ya milioni moia ya wanafunzi wa shule la mwisho ya msingi wameanza tayari hii alhamisi mitihani yao ya kiserkali kote inchini DRC na hasa kunako inchi jirani ambako macenta zingine zili chimikwa, ili kuwapa fursa kupitisha mitihani hii.

Na jimboni Ituri huko Tsere, wataalam wa utafiti ya janga la Ebola wali shambuliwa na wakaaji kabla kwao kuokolewa na jeshi ya ulinzi. Ni kunako maeneo ki afya ya Rwampara.

Na ni kilometa nane itakayo karabariwa na kuwekwa lami huko Mbujimayi jimboni kasai ya mashariki, ikiwa ni ngojeleo ya wakaaji walio teseka siku nyingi na hali ya barabara hii mbovu.

/sites/default/files/2026-06/120626-jrnl-swahili-matin_-_ok.mp3