Habari zetu za jumatano tarehe 30 julay 2025.
- Kuimarisha umoja na usalama wa kijamii kati ya makabila ya wahema na walendu , ndiyo lengo la mkutano mkubwa ulioendeshwa pale ukikusanyisha viongozi wa kabila hizo pale Djugu.
- Kivu ya kusini: wakandideti 27 hawakuweza kufanya mitihani wa serkali kwenye senta ya Mubumbano huko Walungu. Sababu ni vita vinavyo endeshwa mashariki mwa nchi na waasi wa M23, haswa katika eneo la Walungu.
- habari njema kwa wakazi wa kata fulani pale Mbuji-Mayi. Maji ya kunywa yamekuwa yakitiririka mfululizo kutoka kwenye mabomba ya kaya kadhaa. Juhudi hii liliwezeshwa kwa msaada wa Benki ya Maendeleo ya Afrika na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani.
/sites/default/files/2025-07/30072025-journalswahilimatin-00web.mp3





