Habari zetu za Jumane september 2
- Mwaka wa shule 2025-2026 ulifunguliwa rasmi Jumatatu hii, Septemba 1, pale Muanda jimboni Kongo-Kati naye Waziri wa Elimu ya Taifa. Raissa Malu alikiri kwamba hali ya usalama Mashariki mwa congo umevuruga elimu ya maelfu ya watoto, ila haita zoofisha juhudi ya serikali.
- Gavana wa zamani wa kijeshi wa Kivu Kaskazini, Cirimwami Nkuba Peter, alipandishwa cheo na kuwa Luteni jemadari, baada ya kifo chake. baadhi ya wakazi wa Kivu Kaskazini wanasema kukumbuka ukaribu wake afisa huyu mkuu na wakazi.
- Pale Ngandajika katika jimbo la Lomami, familia ishirini na sita (26) zimekuwa zikiishi bila makao tangu Jumamosi iliyopita .Hii ni matokeo ya moto usiojulikana asili yake kujitokeza na kuteketeza nyumba zao.
/sites/default/files/2025-09/02092025-journalswahilimatin-00web.mp3







