Habari zetu za Jumanne september 09
- Uvira, utulivu mdogo umeonekana tangu jioni. FARDC inaonyesha kuwa bado linadhibiti hali katika eneo, baada ya vurugo na maandamano ya watendaji wa mashirika ya kiraia asubui. Kulingana na msemaji wa Operesheni Sokola 2 Kivu Kusini, mtoto wa miaka 12, aliyepatwa na risasi wakati wa fujo hizi, kwa bahati mbaya alifariki dunia.
- Kasai mashariki, SYNAMED Muungano wa Kitaifa wa Madaktari, wanadai malipo halisi na kwa wakati wa mishahara yao. SYNAMED likashifu unyanyasaji unao tendewa kwao na serikali kuu. Na ilitoa makataa ya saa 48 kwa serikali kuboresha hali ya malipo.
- Huko Ituri: karibu tani elfu 35 za kakao tayari zimesafirishwa kwa njia ya kimagendo nje ya jimbo hadi Uganda . Hayo yalitangazwa Jumamosi iliyopita mjini Bunia na Waziri wa Kilimo, Muhindo Nzangi, ambako alijadili kampeni ya kilimo ya 2025-2026.
/sites/default/files/2025-09/09092025-journaswahilimatin-00web.mp3







