Habari za asubui, tarehe 15 juni 2026

Shirika za kutetea haki za binadamu zinaomba uchunguzi huru kuweza kufanyika kuhusu maandamano ya upinzani ya siku ya tano mjini Kinshasa, huku yakikosoa pia matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji.

Jimboni Kivu kaskazini, tarafani Masisi, zaidi ya shule makumi tatu zimefungwa kufuatana na hali ya usalama mdogo na ma elfu ya wanafunzi kukosa masomo na wengine kuweza kuhamishwa centa za mitihani ya kiserkali.

Na huko kasai ya mashariki, ni viongozi katika sekta ya afya ndio wana endelea kampeni ya uhunguzi ya kifua kikuu katika gereza la Mbuji mayi katika lengo la kuweza kuzuwia kuambukizwa kwa wafungwa wengine.

/sites/default/files/2026-06/1506026-journal-swahili-lundi_matin-00_ok.mp3