Tangazo la harakati mpya ya kisiasa yake Joseph Kabila lazua maoni mbalimbali. Mwanabunge wa kitaifa Joseph Nkoy Wembo ametoa wito wa umoja wa kitaifa ili kulinda uhuru na uadilifu wa kijiografia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakati mdadisi wa siasa Christian Moleka anaamini kwamba rais mstaafu sasa amefafanua msimamo wake wa kisiasa.
Ingawaje Kuwapokea wafungwa wapya jelani kuu la Mbanza-Ngungu kumesimamishwa kwa mda wa miezi saba hivi sasa kufuatia mlipuko wa kipindupindu, wafungwa wapya 95 walipokelewa huko Jumapili. Hawa wahamishwa toka jela la Boko, kufwatiya jaribio la kutoroka kwao toka gereza hilo....
Mjini Kinshasa, abiria wa mabasi ya Transco walahumu nauli za 'nusu safari'. Katika baadhi ya njia, madereva husimama kabla ya kituo cha mwisho, na kuwalazimisaha abiria kulipia pesa ya zihada ili kufika wanakoenda.
/sites/default/files/2026-10/14102026-journal-sw-matin-00.mp3







