Journal Soir

Habari za siku ya inne jioni tarehe 08/12/2022

  • Uchunguzi wa awali wa ofisi ya umoja wa mataifa ya haki za binadamu na MONUSCO ulithibitisha kuwa wapiganaji wa M23 waliwaua takriban raia mia moja makumi tatu na moja, wakiwemo wanaume mia moja na wawili, wanawake kumi na saba na watoto kumi na wawili.
  • Kuhusu mauaji haya ya Kishishe, sauti nyingi zinapazwa na kutaka kuona wahusika wa uhalifu huu kufikishwa mahakamani, na hasa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, CPI.
  • Utulivu unaonekana siku ya ine hii karibu katika uwanja wote wa mapigano kati ya FARDC na waasi wa M23 katika tarafa za Rutshuru na Nyiragongo.
  • Katika jimbo la Kivu Kaskazini, wanawake mashuhuri wa Kitshanga wanatoa wito kwa serikali ya mkoa na washirika wake kuandaa kwa haraka mazungumzo ya amani katika mji huo.
  • Katika Ituri, zaidi ya wanamgambo makumi tano wa kikundi cha CODECO kiitwacho Bon Temple de Dieu na wategemezi wao wamekusanywa tangu hii siku ya tatu katika eneo la uchimbaji madini la NZEBI, kilomita mnane  kutoka manispa Mungwalu katika tarafa la Djugu.
  • Wanajeshi wa pamoja wa FARDC-FNDB wa EAC waliwasili mwishoni mwa juma lililopita huko Bijombo, katika mabonde ya tarafa la Uvira. Iko ndani ya mfumo wa awamu ya pili ya operesheni za pamoja za vikosi vya pamoja FARDC-FNDB (jeshi la Burundi). Taarifa iliyotolewa na vyanzo vya pahali imethibitishwa na msemaji wa
  • Katika jimbo la Kivu Kusini, zaidi ya kesi makumi saba na tatu za wahasiriwa wa kike wa unyanyasaji wa nyumbani zimerekodiwa kwa kipindi cha Januari hadi Novemba mwaka tunao./sites/default/files/2022-12/08122022-p-s-journalswahilisoir_-00_web.mp3