Habari za siku ya kwanza jioni tarehe 16/10/2023
- Mahakama kuu yani Cour de cassation ilianza shughuli zake siku ya kwanza hii kwa mwaka wa elfu mbili makumi mbili na tatu na mwaka elfu mbili makumi mbili na inne .
- Jimboni Kivu ya Kaskazini, mji wa Kitshanga, katika eneo la Masisi, uliamshwa na hali ya utulivu siku ya kwanza hii.
- Katika jimbo la Mai-Ndombe, hali ya usalama inaanza kuimarika katika eneo la Kwamouth, ambalo lilikumbwa na ukosefu wa usalama unaosababishwa na wanamgambo wa Mobondo, kufuatia mzozo wa jamii za Teke-Yaka kwa zaidi ya mwaka mmoja.
- Jimboni Ituri, karibu makao mia moja ya wakimbizi wa eneo la Nyamusasi yalisombwa na upepo mkali ulioambatana na mvua siku ya sita katika usulutani wa Bahema Banywagi mtaani Djugu.
- Katika mtaa wa Beni jimboni Kivu ya kaskazini, maeneo manne ya wakimbizi yaliyo katika sehemu ya kaskazini ya mji wa Oicha sasa yanapewa maji ya kunywa. Ni mradi ulioanzishwa na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu CICR .
- Katika jimbo la Tshopo, eneo la afya la Banalia hivi karibuni litakuwa na maji ya kunywa.
- Mjini Tshikapa katika jimbo la Kasai, shirika ya kiraia linaonya juu ya wizi wa taa za barabarani zilizowekwa katikati ya mji kati ya kilalo la Tshikapa na mtaa wa Dibumba ya pili./sites/default/files/2023-10/161023-p-s-kinjournalswahilisoir-00_web.mp3