Habari za siku ya tano jioni tarehe 15/12/2023
- Marekani inatangaza kujitolea kwake kwa kuchukuwa hatua zote ili kuazibu mtu yeyote anayetatiza uchaguzi au kuaribu mchakato huu wa kidemokrasia,
- Uchaguzi wa Rais: mgombea namba makumi mbili na moja , Martin Fayulu aliwasili jana siku ya inne katika mji wa Kikwit jimboni Kwilu.
- Wagombea wawili wa urais walijiondoa na kujiunga na Felix Tshisekedi. Hawa ni Joelle Bilé na Patrice Majondo.
- Huko mjini Mbandaka, wakuu wa polisi mia moja na makumi tano walikamilisha mafunzo yao ya kudumisha utulivu wa ummasiku ya tatu .
- Katika jimbo la Maniema, siku chache kabla ya uchaguzi wa tarehe makumi mbili mwezi wa kumi na mbili, offisi kuu ya CENI jimboni humo inaongeza vikao vya uhamasishaji kwa wakazi.
- Siku tano kabla ya uchaguzi nchini Kongo , mamia ya vieti via uchaguzi vinapatina kwenye ma redio mbalimbali pamoja na ma offisi zingine ya kifedha katika mji wa Bunia.
- Katika jimbo la Tshopo, mafunzo ya toleo la kwanza la wanafunzi wa kijeshi yalimalizika jana.
- Kuhusu Kampeni zidi ya unyanyasaji ya mwanamke , Radio Okapi inaangalia hatua za kimila na desturi katika hali hii.
- Katika jimbo la Kongo Central, kazi ya upakuaji ilimalizika jana katika bandari ya kimataifa ya Matadi ya magari saba yaliyokusudiwa usafiri wa reli./sites/default/files/2023-12/151223-p-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3