Habari za jioni 12 Februari, 2025
- Kinshasa : Ujumbe unaojumuisha wajumbe wa Baraza la Maaskofu wakatoliki la CENCO na Kanisa la Kristo nchini Kongo (ECC) walikutana hii siku ya tatu mjini Goma na Corneille Nanga pamoja na viongozi wengine wa kundi la waasi la M23 ili kuitoa nchi katika mgogoro inayoipitia
- Kinshasa : Kesi kati ya Kongo na Rwanda imefunguliwa hii siku ya tatu tarehe kumi na mbili februari mbele ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu mjini Arusha, inchini Tanzania
- Goma : Huko Kivu Kaskazini, familia nyingi za kijeshi, zilizokuwa zikiishi katika kambi ya kijeshi ya camp Katindo, zilikimbia kambi hii hadi maeneo tofauti ya hifadhi. Hazina msaada wowote hadi sasa/sites/default/files/2025-02/120225-p-s-journalswahilisoir-00-web.mp3