journal soir

Habari zetu za Jumatano tarehe 10 september .

  • Mgomo wa walimu katika maeneo ya Rutshuru, Masisi na Walikale imeimarishwa. Muungano wa walumu Kivu Kaskazini, washutumu kushindwa kutimiza mahitaji ya  walimu, hasa malipo ya mishahara ya walimu katika majimbo ya elimu ya Kivu Kaskazini 1, 2 na 3.
  • Takriban raia 18 waliuawa siku ya Jumanne huko Fotodhu, eneo la kilimo lililoko takriban kilomita kumi magharibi mwa Oicha, mji mkuu wa eneo la Beni. Kulingana na mashirika ya kiraia, idadi ya vifo inasalia kuwa ya muda, kwani wakulima kadhaa hawapo.
  • Wakazi wa Kasai mashariki wametakiwa kuzingatia hatua za usafi ili kuzuia kuenea kwa janga la virusi vya Ebola, kufuatia tangazo la kuonekana tena kwa ugonjwa huu katika mkoa jirani wa Kasai. Mwito huo ni wake Jean Sumba, mtaalamu wa magonjwa katika eneo.

 /sites/default/files/2025-09/10092025-journalswahilisoir-00web.mp3