Journal Soir

Habari za  siku ya tatu jioni ya tarehe 14/06/2023

  • Daktari  kiongozi wa Kituo cha Usambazaji Damu mjini  Butembo anaalika watu wa moyo mwema kutoa damu yao ili kuokowa maisha ya wengine.
  • Na mjini Beni, watu watano watoaji bora wa damu kwa miaka mengi,  walipewa vieti na  heshima  siku ya tatu hii  katika sherehe ya Siku kuu ya Wachangia Damu Duniani.
  • Jimboni Kivu ya Kusini, Shirika  ya kiraia inaelezea wasiwasi wake kuhusu  kazi ya mradi ya maendeleo ya mitaa  mia moja na makumi inne na tano katika jimbo hilo.
  • Huko mjini  Tanger kaskazini mwa Morocco, shirika ya Vyombo vya Habari kwa Uvuvi Endelevu barani Afrika (OMPDA), kwa kushirikiana na muungano  wa Mawaziri wa Ushirikiano wa Uvuvi kati ya Mataifa ya Afrika ya katribu na  Bahari ya Atlantiki, ilizundua  kikao  kuhusu bahari na uvivi siku ya tatu hii .
  • Mkuu wa jeshi wa FARDC aliwasili siku ya tatu hii mjini Kisangani.  
  • Katibu Mkuu makamu  wa Umoja wa Mataifa anayehusika na  suala la ubakaji  unaofanywa wakati wa migogoro anayepatiakna  mjini Goma tangu siku ya pili, alitembelea siku ya pili hiyo , Hospitali ya Heal Africa mjini Goma.
  • Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini: mwanamke ambaye alishtakiwa  kuua mtoto, alihukumiwa kwa azabu ya kifo siku ya pili na mahakama ya kijeshi ya mji wa Goma.
  • Muungano wa kitaifa wa vyama vinavyopigana dhidi ya mimba zisizotamaniwa  unaomba kuondowa adhabu  kuhusu jambo la kuondowa  mimba nchini kongo ya kidemokratia kufuatana  wa azimio ya Maputo./sites/default/files/2023-06/140623-p-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3