Habari za mangaribi, siku ya tatu 150426
- Shirika la kutetea haki za binadamu, la Human Rights Watch, lime tangaza Siku ya tatu hii kwamba, katika nyanda za juu za Kivu Kusini, wanajeshi wa Kongo na makundi yenye silaha, yanazuia utoaji wa misaada , na kuwazuia raia kukimbia mapigano , mashariki mwa Congo.
- Jimboni Kivu kusini, Vituo tano vya afya Katika maeneo ya Uvira na Fizi jimboni , vinakabiliwa na janga, la kipindupindu.
- Katika jimbo la Kasai central , Shirika la Kazi Kuu la Kongo (ACGT), ambalo linasimamia kazi ya ukarabati wa barabara ya Kananga-Kalamba Mbuji , kwa niaba ya serikali ya Kongo, inaripoti kuwa , kazi , inaendelea vizuri.
- /sites/default/files/2026-04/150426-journalswahili-mercredisoir-00_web.mp3





