Maandamano ya UDPS/Tshisekedi kwa kuunga mkono kiongozi wa taifa ilifanyika Jumanne katika jimbo kadhaa za DRC. Kinshasa, waandamanaji walianza kutoka barabara ya 11 ya Limete wakiongozwa hasa na Katibu Mkuu wa chama, Augustin Kabuya, pamoja na wakurugenzi wengine wa UDPS.
Jimboni Kasai ya Kati, moto ilisababisha hofu Jumatatu mjini Kananga. Kwenye barabara la Daktari Étienne Tshisekedi, yenye kuitwa zamani Makar, maghala mawili ya biashara yaliteketezwa na moto.
Na Kivu ya kaskazini, wiki tatu baada ya kuanza kwa shule, shule nyingi katika groupement ya Mwenye, eneo la Lubero zinakuwa na shida nyingi kwa kuanza masomo. Tatizo ni ukosefu wa usalama wa kudumu katika sehemu hii ya eneo ambapo wakaaji wengi hawaya rudi vijijini vyao.
/sites/default/files/2026-09/23926-b-s-journal_swahili_mercredi_matin_.mp3







