Jimboni Ituri, bado, wagonjwa wanao fika kwenye Kituo cha Matibabu ya Ebola pa Nyakunde ni wachache. Hata waganga wamoja hawajarejea kazini katika kituo hicho kinacho patikana kwa umbali wa kilometa 45 na mji wa Bunia. Hali hii yatokana na machafuko yaliyolikumba eneo hilo hivi karibuni.
Na jimboni Kivu kusini, Uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Kahuzi-Biega (PNKB) umelaani mauaji ya sokwe, yaani gorille ya aina Grauer. Aliye tenda kitendo hicho tayari amekamatwa na kupelekwa mbele ya sheria.
Maafisa sitini wa polisi wa mahakama kutoka Kasaï-Central, wamemaliza mafunzo mjini Kananga. Mafunzo haya yalihusu namwa ya kuendesha Uchunguzi bora kwa ajili ya haki bora.
/sites/default/files/2026-07/21072026_-_jp_sw_-_soir_-_00.mp3







