Journal Swahili Soir, 22 Juillet 2026.

Jimboni Ituri, wakaaji wamesimamisha kazi zao katika eneo la Mahagi tangu siku ya pili. Ni kutokana na wito wa mashirika ya kirahiya ili kupinga unyanyasaji unaofanywa na baadhi ya maafisa wa polisi wa trafiki pamoja na hali ya usalama inayozidi kuzorota katika eneo hilo.  

Mbuji-Mayi, Wanawake wanaosumbuliwa na tatizo la fistula ya uzazi wanaalikwa kufika katika Kituo cha Hospitali ya Presbyterian ili kupata matibabu ya bure. Mpango wa matunzo ulio anza siku ya tatu, utaendelea hadi mwisho wa mwezi Agusti.

Jimboni Kivu kaskazini: Shirika la raiya lanalaumu vitendo wanavyo tendewa wakaaji jimboni humu na vikundi vishikavyo silaha. Ikiwa ni pamoja na mauaji ya halaiki, utekaji nyara, uporaji, na na kulazimisha wakaaji kuorozwa katika vikundi mbalimbali vya vita.

/sites/default/files/2026-07/22072026_-_journal_swahili_-_soir_-00.mp3