Journal matin

Habari za siku ya tatu asubuhi 

  • Serikali imechukua chaguo la kujenga magereza mapya ili kupunguza msongamano na hali mbaya ya magereza.
  • Huko Ituri, zaidi ya wafungwa makumi mbili na watano wamefariki katika gereza kuu la Bunia katika muda wa miezi miwili iliyopita.
  • Kuna mvurugiko katika chama cha urais cha Udps ambapo Victor Wakwenda, mkuu  wa Chama cha Convention démocratique du parti (CDP) aliachiliwa huru kwa muda baada ya kufika katika ukumbi wa baraza mbele ya Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu karibu na Mahakama ya Rufaa ya Kinshasa-Matete katika gereza kuu la Makala siku ya pili hii makumi mbili na mbili  Novemba.
  • Wakikimbia vita, jamaa za wakimbizi zilikaa katika maeneo tupu katika tabaka Kibati katika tarafa la Nyiragongo.
  • Katika mji wa Bandundu, mji mkuu wa jimbo la Kwilu, washambuliaji kadhaa wenye silaha waliokamatwa katika tarafa la Bagata walionyeshwa siku ya kwanza na polisi wa kitaifa wa Kongo kwa gavana wa mkoa, Willy Itshundala Assang
  • Katika Kivu Kusini, watu kumi wamekufa na uharibifu mwingine mwingi wa vitu. Ni matokeo ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea katika  usiku wa kuamukia siku ya pili hii huko Kamituga, tarafa la Mwenga.
  •  
  • Katika jimbo la Bas-Uélé, Mkuu wa Ofisi Ndogo ya OMS/Kisangani anasihi kuhusika kwa kiongozi tawala wa eneo katika kuandaliwa kwa awamu mbili za mwisho za kampeni ya uimarishaji ya mara kwa mara ya chanjo za utaratibu, IPVS katika eneo hili.
  • Katika jimbo la Lomami, imewasili siku ya kwanza  kwa mara ya kwanza kabisa pa Mwene-Ditu, basi kutoka kampuni ya usafiri ya Congo Transco./sites/default/files/2022-11/231122-p-s-journalswahilimatin-00_web.mp3