Journal matin

Habari za siku ya inne asubuhi 

  • Mkutano mdogo wa Luanda ulifanyika bila kuwepo kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye aliwakilishwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje Vincent Biruta, vyombo vya habari vya rais wa Kongo vilisema katika tangazo.
  • CENI inaanza mabadiliko muhimu katika mchakato wa uchaguzi kuanzia mwezi Disemba ijayo kwa uendeshaji wa utambuzi na usajili wa wapiga kura nchini DRC.
  • Treni ya uchaguzi itaanza mwezi ujao operesheni ya kuanzisha faili mpya ya wapiga kura inayotegemewa na inayojumuisha wote, kulingana na mkuu wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi.
  • Katika Kivu Kusini, mvutano mkali unaonekana kwa sasa kati ya manaibu wa mkoa na bunge la mkoa wa Kivu Kusini.
  • Katika jimbo la Tshopo, Waziri wa Uchukuzi na njia za mawasiliano alizindua rasmi hii siku ya kwanza mjini Kisangani, kazi za ukarabati wa uwanja wa ndege wa Banbgoka.
  •  Katika Kwilu, wakulima wa tarafa la Bulungu wanapata matatizo makubwa katika kuhamisha mazao yao ya kilimo, ambayo ni mihogo, mahindi, karanga na mengine, hadi vituo vya matumizi vikiwemo mji wa Kikwit, Kinshasa na maeneo mengine.
  • Sehemu nyingi za DRC zimevurugika kutokana na mvua kubwa inayonyesha na kusababisha vifo vya makumi ya watu, nyumba zilizoharibiwa na maji ya mvua, mafuriko, barabara zilizokatwa na uharibifu mwingine mwingi.
  • Katika Kasaï-Oriental, wiki mbili baada ya kuwasili kwa Mbuji-Mayi kwa mabasi tano kutoka kampuni la Société de Transport du Congo, Transco kwa kifupi, hakuna mpango hadi sasa ambao umetangazwa kuhusu usafiri wa watu katika jiji hilo./sites/default/files/2022-11/24112022-p-s-journalswahilimatin-00_web_.mp3