Journal matin

Habari za siku ya kwanza asubuhi tarehe 05/12/2022

  • Awamu ya tatu ya mchakato wa amani mashariki mwa DRC itamalizika siku ya kwanza hii katika hoteli ya Safari Park jijini Nairobi.
  • Waziri Mkuu Sama Lukonde alikabithi Waziri wa Masuala ya Kijamii, Mshikamano na Hatua za Kibinadamu, Modeste Mutinga siku ya kwanza hii tarehe tano Desemba, hapa Kinshasa, kartasi ya kuchukua pesa kwenye bengi yenye Franga za Kongo bilioni mia mbili.
  • Huko Kivu Kaskazini, utulivu ulionekana  wikendi yote, hadi siku ya kwanza hii kwenye uwanja wa mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la Kongo.
  • Askofu wa dayosisi ya Katoliki ya Butembo-Beni anasema ana wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya usalama katika mji wa Butembo.
  • Jimboni Ituri, askofu wa  dayosisi ya katoliki ya Bunia analaani uporaji wa rasilimali za jimbo hilo unaofanywa na wageni na baadhi ya Wakongo. Kulingana na Askofu Dieudonné URINGI, hawa wanachukua fursa ya vita kujitajirisha kinyume na sheria wakati wakazi wanaishi kwa taabu.
  • Kampeni ya Siku kumi na sita za Kupinga Ukatili wa Kijinsia inaendelea bila kusitishwa kote nchini.
  • Miezi miwili hivi, mafuriko yanaendelea kuvuma katika maeneo mengi ya Equateur. Ni kutokana na mvua kubwa inayonyesha kila siku katika eneo hilo.
  • Huko Kasaï-Oriental, bei ya mahindi imeongezeka katika masoko ya jiji la Mbuji-Mayi./sites/default/files/2022-12/05122022-p-s-journalswahilimatin-00_web.mp3