Journal Soir

Habari za siku ya tano jioni 

  • Jimboni Ituri, askari jeshi wa Monusco wanafanya ulinzi wa takriban wakimbizi elfu mia moja makumi mbili katika maeneo mbalimbali tarafani Djugu.
  • Katika jimbo la Kivu kusini,  kuhamasisha viongozi wa vyama vya kisiasa kwa kuzingatia uchaguzi ujao, na kuhusu jukumu la Monusco, hiki ndicho kikubwa cha mkutano ulioandaliwa Bukavu hii siku ya ine tarehe kumi na tatu oktoba mwaka tunao.
  • Kivu Kaskazini: bunge la vijana la mji wa Beni limejitolea kupambana na taarifa zisizo sahihi  katika jamii na kupitia mitandao ya kijamii.
  • Bunge la Kitaifa liliruhusu  jana siku ya ine, bila mjadala,  na wingi wa manaibu mia tatu makumi nane na tatu kati ya mia tatu makumi nane na sita  waliokuwepo, kuongezwa kwa mara ya makumi tatu na ine uongozi wa kijeshi katika majimbo ya Ituri na Kivu Kaskazini.
  • Jimboni  Kivu ya Kaskazini, Kikosi cha Kitaifa cha Wafanyakazi, Fosynat, kinapinga kukamatwa na kushikwa kiholela kwa baadhi ya walimu na idara za kijasusi katika majimbo
  • Mjini Kinshasa, wakaaji wa nyumba zilizojengwa katika shamba la wafu la Kinsuka katika manispa Mont Ngafula wana chini ya wiki moja kuondoka kwenye maneneo hayo.
  • Takriban wanawake mia tatu walio katika mazingira magumu wananufaika na mradi wa uwezeshaji wao kiuchumi katika jimbo la Kivu kusini.
  • Dunia nzima inaadhimisha tarehe kumi na tano oktoba ya kila mwaka, Siku ya Kimataifa ya mwanamke wa kijijini./sites/default/files/2022-10/1410022_-p-s-journalswahilivendredisoir-00_web.mp3