Journal Soir

Habari za siku ya inne jioni 

  • Katika jimbo la  Kivu Kaskazini, hali bado ni ya wasiwasi siku ya ine hii katika tabaka Rugari, kilomita makumi ine  kaskazini mwa Goma.
  • Zaidi ya familia elfu kumi na sita za wakimbizi waliokimbia mapigano ya hivi majuzi kati ya jeshi la FARDC na waasi wa M23 wanapokea msaada wa chakula kutoka kwa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, PAM kwa kifupi.
  • Jimboni Ituri, kurushiana risasi kuliripotiwa katika usiku wa kuamukia hii siku ya ine kati ya wanamgambo waasi wa kundi lenye silaha la FRPI  na askari jeshi la wanamaji wa Uganda kwenye Ziwa Albert, haswa zaidi kwenye kisiwa cha Matete katika tarafa la Irumu huko Ituri.
  • Visa vingi vya kuhara na kutapika vimerekodiwa katika mji wa Likasi huko Haut Katanga. Watu wawili tayari wamekufa.
  • Chanjo ya watoto imeanzishwa siku ya ine hii katika mitaa ya afya kumi na nane Équateur dhidi ya mugonjwa wa polio.
  • Katika jimbo la Maniema ambapo hali ya  barabara ni mbaya katika tarafa la Kailo.
  • Shirika la Union de commissionnaires en douane agréé du Tanganyika, UCODAT Tanganyika, wanalaani wingi wa kodi katika bandari ya Kalemie.
  • Barabara Bypass sasa inanufaika kutokana na mwangaza wa umma kwenye sehemu yake kati ya l’Echangeur de Limeté na njiapanda Ngaba./sites/default/files/2022-11/101122-p-s-journalswahilisoir-00_web.mp3