Journal Swahili Soir, 28 Juillet 2026.

Kamina, katika jimbo la Haut – Lomami, Rais Félix-Antoine Tshisekedi anatarajiwa Kamina siku ya tatu hii, huku viongozi wa eneo hilo wakiendelea na maandalizi ya kumpokea.

Ituri : Malalamiko ya wasafiri yanaendelea Ituri kuhusu malipo ya lazima kwenye vizuizi vya barabarani licha ya agizo la kuondolewa kwa vizuizi visivyo halali.

Katika jimbo la Maniema, gereza kuu la Kindu linakabiliwa na mlipuko wa tete-kuwanga, yaani varicelle huku takribani wafungwa kumi wakiwa wameambukizwa ugonjwa huo. 

/sites/default/files/2026-07/280726-p-s-journal_complet_mardi_soir-00.mp3