Mashirika yasiyo ya kiserikali yalaani kushindwa kutii makubaliano ya Washington na Doha; huku, mashirika haya yataka kushiriki kwa karibu zaidi katika juhudi za amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Viongozi wa madini sasa wanachukua jukumu kikamilifu katika mapambano dhidi ya Ebola inchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Walipokutana Alhamisi mjini Kinshasa, kwa mpango wa Caritas Congo ASBL, waliandaa ramani ya pamoja inayoweka majukumu maalum na tarehe za mwisho.
Jimboni Kivu Kaskazini, mtaani Rutshuru, Wanafunzi kadhaa hawasomi kijijini Bwalanda, usultani wa Bwito, kwa mda wa siku tatu sasa. Hii ni matokeo ya mvua kubwa yenye upepo mkali iliyokumba eneo hilo Jumanne na kuharibu shule mbili za mahali.
/sites/default/files/2026-10/021026-journal-swahili-vendredi-00.mp3







