Alphonse Kambale, Mjumbe wa gavana pa Nyamilima katika tarafa la Rutshuru, jimboni Kivu Kaskazini

Hali ya usalama pa Nyamilima, katika tabaka Binza, katika tarafa la Rutshuru, bado inatia wasiwasi licha ya utulivu uliopo. Kufungwa kwa kambi ya MONUSCO, wakati wanajeshi wako katika operesheni dhidi ya M23 huko Bunagana, kunatia wasiwasi raia kwa kiasi fulani. Wanahofia kwamba makundi yenye silaha yanayoizunguka yanaweza kuchukua fursa ya hali hii na kuzidisha unyanyasaji. Alphonse Kambale, mjumbe wa gavana pa Nyamilima, ndiye mgeni wetu. Anazungumzia hali hiyo katika mahojiano haya na Sifa Maguru.  

/sites/default/files/2022-11/09._021122-p-f-invitekisanganikis_invite_vlf_fr_web_0.mp3