Katika jimbo la Kivu ya Kusini, chama cha wavuvi wa Ziwa Kivu kinaonya juu ya hatari yakupoteya kwa aina ya samaki wanaoitwa Sambaza ikiwa hakuna kitakachofanyika kwa haraka . Uvuvi wa samaki hii imeshuka sana .Miongoni mwa sababu, wataalam wa uvuvi wanataja uharibifu wa mazingira na ukosefu wa usalama katika Ziwa Kivu. Mwanabunge jimboni Fredy Maisha chaguliwa wa eneo la Idjwi alipendekeza kwa liwali wa jimbo wa mkoa kuandaa mkutano unaokutanisha watu wote wanaohusika na uharibifu wa mazirngira katika Ziwa Kivu. Mkutano huo ulifanyika mnamo tarfehe tatu mwezi huu wa kumi na moja mjini Bukavu katika chumba cha INPP. Fredy Maisha anazungumza kuhusu suala hilo na Jean Kasami./sites/default/files/2022-11/inviteswahilideputemaisha-web.mp3